Na Eva Godwin-DODOMA
MENEJA wa Taasisi ya TASESO, Kwido Julius Sanga amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kupendekeza kufutwa kwa ada kuanzia kidato cha Tano mpaka cha Sita wakati Waziri Mwigulu Nchemba akiwasilisha bajeti ya Nchi Jana Jijini Dodoma.
Akizungumza na Waandishi wa habari June 15,2022 jijini Dodoma katika kikao cha kuwapongeza serikali katika sekta ya elimu.
Amesema Serikali hii ya awamu ya sita imekuwa ya kitofauti kuanzia kwenye suala la Sensa mpaka suala la Elimu.
“Mama yetu anaupiga Mwingi katika sekta ya elimu na hata hivyo Familia ya watu wanaoishi mazingira magumu watapata fursa ya kusoma”,Amesema Sanga
“Hii itawasaidia sana watoto wanaoishi mazingira magumu hakuna Mtoto hatakae weza kubaki nyumbani kwa suala la ada labda liwe jambo jingine”
Hata hivyo amewaomba wananchi Mkoa wa Dodoma kuonyesha ushirikiano kwa Maafisa katika suala zima la Sensa.
“Sensa hii imekuwa ni yatofauti na haijawai kutokea kwasababu hii ni Sensa ya Majengo na haijawai kutokea tangu tumepata Uhuru katika Nchi yetu
“Hivyo tunaomba ushirikiano wenu kwa Maafisa ili suala liende kama tulivyokusudia siku hiyo itakayowadia”.Amesema Sanga