Burudani Featured

HALIMA KOPWE MISS TANZANIA , RAIS SAMIA KUJENGA UKUMBI WA KIMATAIFA JIJINI DAR

Written by mzalendoeditor

Na John Mapepele

Waziri
wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Mhe, Mohamed Mchengerwa amesema
Serikali ya Mhe. Rais Samia imedhamiria kuinua kuinua kiwango cha
mashindano ya urembo nchini  ikiwa ni pamoja na kujenga ukumbi wa
kimataifa  katika jiji la Dar es Salaam.
Akizungumza
usiku wa kuamkia leo Mei 21, 2022 kwenye kilele cha mashindano ya
kumtafuta  Miss Tanzania 2022 ambapo Halima Kopwe toka Mtwara ametwaa
taji hilo, Mhe . Mchengerwa amesema ukumbi huo  licha ya kufanyiwa kazi
mbalimbali za Sanaa na burudani pia utatumika kwenye mashindano ya
kimataifa ikiwa ni pamoja na shindano la Miss Tanzania.
 “Ukumbi
huo unatarajiwa kuongoza kwa ubora na ukubwa barani Afrika ambapo
utachukua takribani watu elfu ishirini” amesisitiza Mhe. Mchengerwa
Aidha,
amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendelea kuwashika mkono washindi
wote na kufafanua kuwa washiriki wote walioshiriki shindano hili hadi
kufika fainali ni washindi.
Amewapongeza
waandaji wa shindano hilo kwa uratibu mzuri  ambapo ameongeza kuwa
washiriki  wamefanya kazi nzuri ya ubunifu na Sanaa.
Pia amesema Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ndiyo Wizara pekee inayowapa furaha na faraja watanzania wengi.
Pia
Mhe. Mchengerwa amesema Filamu ya Royal Tour imesaidia kufungua milango
na kuitangaza Tanzania  duniani na kuwataka wasanii kutumia fursa hiyo
kutengeneza ajira na vipato.
Miss
Tanzania kwa mwaka huu; Halima Kopwe amejishindia gari  dogo aina ya
Benzi lenye thamani ya shilingi milioni 30 na  fedha taslimu shilingi
milioni kumi.
Shindano hilo limefanyika jijini Dar es Salaam kwenye Ukumbi wa Mlimani City na kuhudhuriwa na mamia ya washabiki wa urembo.

About the author

mzalendoeditor