Featured Kitaifa

OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA YAMPOKEA KATIBU MPYA

Written by mzalendoeditor

katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw,Hassan Omani Kitenge awasili Sekretarieti ya Ajira.

Kaimu Katibu Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma  Mhandisi Samwel Tanguye akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Utawala Bw.Innocent Bomani wakimkaribisha Katibu alipowasili ofisini hapo

…………………………………………………..

OFISI YA RAIS SEKRETARIETI YA AJIRA KATIKA UTUMISHI WA UMMA YAMPOKEA KATIBU MPYA

Katibu wa Ofisi ya Rais Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma  Bw.Hassan Omani Kitenge  ameripoti katika  Ofisi za Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma baada ya kuteuliwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan kushika nafasi hiyo.

Bw.Kitenge amechukua nafasi ya Bw Xavier Daudi ambaye kwa sasa ni  Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora . Akizungumza na Watumishi wa Ofisi hiyo Katibu kitenge amesema kuwa jukumu kubwa la Taasisi ni kuajiri na imebeba dhamana kubwa katika utumishi wa umma.

Aidha, Bw.Kitenge amesema maono  ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan  ni kupata watumishi wa umma wenye  uadilifu,,wenye sifa na wenye kuwajibika kwa hiari ambao ndio watakaosukuma gurudumu la nchi kwenda mbele.

 Bw.Kitenge amewataka watumishi  hao kuchapa kazi kwa  bidi  na kumpa ushirikiano ili kwa pamoja waweze kuyafikia maono  ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan. Kabla ya uteuzi  Bw.Kitenge alikuwa Mkurugenzi wa Mikataba ya Utendaji kazi Serikalini, ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.

About the author

mzalendoeditor