Featured Kitaifa

ZAIDI YA WANAFUNZI 4000 TANGA WANUFAIKA NA MAFUNZO YA SAYANSI KWA VITENDO

Written by mzalendoeditor

Mwezeshaji  wa mafunzo ya Sayansi na teknolojia katika kituo cha 
Sayansi cha Stem Park Shaukatali Hussein  akiwafundisha wanafunzi wa
shule za msingi  na sekondari  katika kituo hicho wakati  wa maadhimisho
ya wiki ya ubunifu mkoani Tanga

Mwezeshaji  wa mafunzo ya Sayansi na teknolojia katika kituo cha 
Sayansi cha Stem Park Shaukatali Hussein  akiwafundisha wanafunzi wa
shule za msingi  na sekondari  katika kituo hicho wakati  wa maadhimisho
ya wiki ya ubunifu mkoani Tanga

Wanafunzi wa
shule za msingi  na sekondari  wakifuatilia mafunzo hayo katika kituo hicho wakati  wa maadhimisho
ya wiki ya ubunifu mkoani Tanga

NA OSCAR ASSENGA,TANGA.

ZAIDI ya  Wanafunzi  wapatao
elfu nne ‘4000’ kutoka shule za Msingi na Sekondari zilizopo ndani ya
mkoa wa Tanga  pamoja na wale waliomaliza na walio nje ya mfumo wa elimu
wameendelea kunufaika na mafunzo ya Sayansi  kwa vitendo yanatolewa na
kituo cha Sayansi cha Sterm Park kwa lengo la kuwaongezea uelewa ikiwa
pia ni njia ya kuwawezesha  kujiajiri kidijitali.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa kituo hicho Max George
wakati wa maadhimisho ya wiki ya ubunifu hapa nchini kwa mkoa wa Tanga
ambapo kupitia kituo hicho wanafunzi wa ngazi tofauti na vijana
waliohitimu masomo kidato cha nne na waliopo nje ya mfumo wa elimu 
wamekuwa wakinufaika  .

George alibainisha kuwa kumekuwa na changamoto kwa baadhi
ya Vijana ambao wapo nje ya mfumo wa elimu pamoja na wale ambao
wameshamaliza elimu ya kidato cha nne kujiendeleza kielimu  ambapo
katika kuhakikisha nao wanapata elimu  hiyo kwao vitendo wamefanya
utaratibu wa kuwaingizia kwenye mfumo rasmi.

“Mpaka sasa tunashukuru muamko wa vijana ni mkubwa  na
tumekuwa tukifanya kazi na shule zote za Jiji la Tanga ambapo tumeingia
kwenye mfumo rasmi ambao unatuwezesha sisi na walimu kufanya kazi  kuwa
pamoja , wao wakiwa wanaofundisha kwa nadharia sisi tunafundishwa kwa
vitendo na  mpaka sasa wanafunzi wapatao elfu nne wamenufaika na mafunzo
tunayotoa” alisema George.

 Aliongeza kuwa  kutokana jiographia ya mkoa wa Tanga ili
kuwafikia wanafunzi wengine waliopo wilaya nyingine wamekuwa
wakizitembelea ili kuhakikisha elimu hiyo inawanufaisha vijana wengi
zaidi na kuondokana na tatizo la ajira ambalo limekuwa ni changamoto wa
kundi kubwa la vijana.
hapa nchini, 

” Changamoto ni kwa vijana ambao wapo nje ya elimu na ambao
hawajabahatika kabisa kwenda shuleni lakini kituo kinawahudumia katika
kuwapa mafunzo ya program mbalimbali za kompyuta maeneo mengine nje ya
jiji la Tanga tunafanya utaratibu kutembelea  shule kwaajili ya kuwapa
elimu hii” alisema Meneja huyo.

Kwa upande wake  meneja wa mradi wa Project Insipire
unaohamasisha kujifunza masomo ya sayansi  katika kituo hicho Dkt Issaya
Ipyana aliwataka wanafunzi wa kike kupenda masomo ya sayansi na
kuachana na dhana ya kuyaona masomo hayo ni magumu.

Dkt Ipyana alisema kuwa wazazi  na walezi wanazidi
kuhamasika kwa kuwaleta watoto wao kujifunza katika kituo hicho huku
akiongeza kuwa  kama wanafunzi wa kike wakipewa mbinu mapema za kuyajua
masomo ya sayansi inaweza kuwasaidia kuipenda sayansi na kuwasaidia
kwenye maisha yao ya baadaye. 

“Dunia inaelekea kwenye mlengwa wa Sayansi na Teknolojia na
mtoto wa kike ana nafasi kubwa hivyo tukiwapa nafasi kujifunza masomo
ya Sayansi itawasaidia mbeleni tofauti na sasa walivyo kwenye jamii”
alisema Dkt Ipyana.

“Sasa tunaelekea ulimwengu wa Sayansi na kidigital hivyo
kupitia mafunzo haya tunawajengea uwezo walimu pamoja na wanafunzi
kupata uwezo na kujua kuwa kuna fursa kupitia ulimwengu wa utandawazi
ambazo zinaweza kuwa njia ya kujiajiri”  aliongeza

Kwa upande wao wanafunzi akiwemo Sarah Michael na Hatuna
Iddi wanaoshiriki programu hizo walisema kuwa  zinawapa mwanga na
kuwawezesha kuyapenda masomo ya sayansi huku wakiwaomba wazazi na walezi
kuwawezesha kuwapatia vifaa vya kujifunzia ili kuwaongezea uelewa
zaidi. 

Hatua hiyo inafuatia wimbi la watoto wa kike kukimbia
masomo ya sayansi jambo ambalo linawafanya wadau mbalimbali kuona
umuhimu wa kuwekeza kwenye eneo hilo ili jamii iachane na hofu ya
kujifunza masomo hayo.

About the author

mzalendoeditor