Featured Kitaifa

‘TUTASIKILIZA WAATHIRIKA WA UKATILI WA KIJINSIA NCHI NZIMA’-WAZIRI GWAJIMA

Written by mzalendoeditor
 
 

 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima, akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Jasinta Mboneko pamoja na Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mwajina Lipinga, wakisikiliza baadhi ya Waathirika wa matukio ya ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto waliojitokeza kufuatia wito wa Waziri huyo jana Aprili 23,2022 akizungumza na kituo cha Redio Faraja mkoani Shinyanga.
 
Waziri Dkt. Gwajima yupo mkoani Shinyanga kukagua shughuli mbalimbali za Wizara hiyo ikiwepo kuona juhudi za vita dhidi ya ukatili wa kijinsia hususani afua zinazotumika kukabiliana vitendo hivyo.
 
Mpango huu wa kusikiliza kero sugu za jamii dhidi ya ukatili wa kijinsia na ukatili wa watoto utaendelea katika ziara zake zote nchini.

About the author

mzalendoeditor