IMERIPOTIWA kuwa Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola, amepewa ofa ya mshahara wa pauni milioni 10 kwa mwaka (Sh bilioni 30 na milioni 228) ili akubali kuifundisha timu ya taifa ya Brazil.
Brazil watakabiliwa na ushindani kwa kuwa Shirikisho la Soka la Uholanzi nalo linamwania kocha huyo mwenye miaka 51.
Guardiola ana mkataba na Man City hadi 2023 na inawezekana akamaliza miaka yake ya mafanikio klabuni hapo.
Kocha wa sasa wa Brazil, Tite, tayari ameshathibitisha kuwa ataondoka katika timu hiyo baada ya Kombe la Dunia 2022 nchini Qatar, na sasa Brazil inasaka mrithi wake.
Kwa mujibu wa Marca, chama cha soka cha Brazil kinaona Guardiola ndiye mtu sahihi anayetakiwa kuinoa timu yao ya taifa.