Featured Michezo

YANGA,SOMALIA HAKUNA MBABE MECHI YA HISANI CHAMAZI

Written by mzalendoeditor
MABINGWA wa kihistoria Tanzania bara Yanga SC imeshindwa kutamba baada ya kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na timu ya taifa ya Somalia katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Azam Comolex, Chamazi nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam.
Zakaria alianza kuifungia Somalia dakika ya 18, kabla ya Mkongo Chico Ushindi kuisawazishia Yanga dakika sita baadaye.
Mchezo  huo ulikuwa maalum kuchangia taasisi ya Ally Kimara Foundation, kijana anayesumbuliwa na maradhi adimu aliyeanzisha mfuko huo kusaidia watoto wengine wote wnaosumbuliwa na maradhi hayo.
Mapema kabla ya mchezo huo,  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan alipiga simu na kuahidi kuchangia Sh. Milioni 15.

About the author

mzalendoeditor