Featured Kitaifa

KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI, KIFUA KIKUU NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA YATEMBELE GEREZA KUU BUTIMBA MWANZA

Written by mzalendoeditor

Naibu Waziri Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Christopher Kadio pamoja na Naibu Kamishna wa Magereza, Jeremia Katungu wakati wanawasubiria Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya Masuala ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Magonjwa yasiyoambukiza kuwasili Gereza Kuu Butimba mkoani Mwanza.

Naibu Waziri Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akiwaongoza Viongozi na Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Magonjwa yasiyoambukiza ambao baadhi yao ni Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati walipotembelea Gereza Kuu Butimba kuonana na wafungwa na mahabusu kujua hali zao na huduma wanazozipata kwenye masula ya UKIMWI.

Naibu Waziri Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini(wanne kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Magonjwa yasiyoambukiza Mhe. Fatma Taufiq (Mb.) (Watano Kushoto) pamoja na wajumbe wa kamati hiyo baada ya kutembelea Gereza Kuu Butimba kuonana na wafungwa na mahabusu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya masuala ya Ukimwi, Dawa za Kulevya, KIfua Kikuu na Magonjwa yasiyoambukiza Mhe. Fatma Taufiq (Mb.) akiongoza kikao cha Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya UKIMWI yanayoendelea leo katika ukumbi wa Mwanza Hoteli leo, Mkoani Mwanza. Pembeni kushoto ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Jumanne Sagini.

Naibu Kamishna wa Magereza, Jeremia Katungu akiwasilisha Taarifa kuhusu Hali ya Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na Upatikanaji wa Tiba kwa Magonjwa nyemelezi na Udhibiti wa Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya Gereza Kuu Butimba kwa Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Magonjwa yasiyoambukiza ambao pia ni Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, katika ukumbi wa Mwanza Hotel, Mkoani Mwanza.

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akijibu hoja za Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge Masuala ya Ukimwi, Kifua Kikuu na Magonjwa yasiyoambukiza ambao pia ni Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo, baada ya Naibu Kamishna wa Magereza, Jeremia Katungu kuwasilisha Taarifa kuhusu Hali ya Maambukizi ya Virusi vya UKIMWI na Upatikanaji wa Tiba kwa Magonjwa nyemelezi na Udhibiti wa Biashara na Matumizi ya Madawa ya Kulevya Gereza Kuu Butimba.

About the author

mzalendoeditor