Featured Kitaifa

SERIKALI YAJA NA MWAROBAINI KUWAONDOA WATOTO WA MITAANI NA KUZUIA UKATILI MAJUMBANI

Written by mzalendoeditor

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), kilichofanyika leo Februari 26,2022 jijini Dodoma.

Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Ali Khamis akieleza jambo wakati wa ufunguzi wa kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), kilichofanyika  leo Februari 26,2022 jijini Dodoma 

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Zainab Chaula akieleza lengo la kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili kwa Wanawake na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma 

KAIMU Mkurugenzi Mkaazi wa Plan International Peter Mwakabwale, akielezea jinsi wanavyotekeleza kwa kushirikiana na  Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili kwa Wanawake na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma 

 Mkurugenzi wa Idara ya Uratibu wa Mashirika Yasiyo ya Kiserikali Vickness Mayao akieleza jinsi Mashirika Yasiyo ya Kiserikali anavyoshirkiana katika afua za kutokomeza ukatili wakati wa kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili kwa Wanawake na Watoto kilichofanyika jijini Dodoma.

MBUNGE wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia Tanzania (NGOs) Neema Lugangira,akizungumza katika kikao kazi cha Wadau wanaotekeleza afua za kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto,kilichofanyika leo Februari 26,2022 jijini Dodoma

 Baadhi ya washiriki wa kikao kazi cha Wadau wanaotekeleza afua za mpango kazi wa Taifa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) wakifuatilia matukio mbalimbali katika kikao hicho kilichofanyika jijini Dodoma 

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima,akiitunza Kwaya ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum wakati ikitumbuiza kwenye ufunguzi wa kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), kilichofanyika jijini Dodoma  

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua  kikao kazi cha Wadau kuweka Mkakati wa kuimarisha utekelezaji wa afua za kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA), kilichofanyika jijini Dodoma  

………………………………………………………

Na Alex Sonna-DODOMA

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima,amewataka wadau kushirikiana na Serikali kufanya oparesheni maalum ya kuwaondoa watoto wa mtaani na kuzuia ukatili majumbani.

Dk.Gwajima ameyasema hayo leo Februari 26,2022 jijini Dodoma wakati akifungua kikao kazi na Wadau waotekeleza afua za kupambana na vitendo vya ukatili nchini.

 Waziri Dkt. Gwajima amesema pamoja na kuwepo Mpango Kazi wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto yaani (MTAKUWWA) bado changamoto ya vitendo vya ukatili inaendelea hivyo wadau wanatakiwa kuunganisha nguvu katika kuhakikisha vitendo hivyo vinatokomezwa.
“Tuje na mbinu za kuondoa haya tumechoka kulala kuwaza mtaani kuna mtoto kakatiliwa muda huu, wengine wana wazazi ili kuepuka kuongezeka na wahanga wa vitendo vya ukatili.”amesema Dk.Gwajima
Waziri Gwajima amesema kuwa kama kuna mzazi ambaye mtoto wake yupo mtaani akatoe taarifa na kwa kamati ya kutokomeza ukatili ya mtaa ili atangazwe.

Amesema kuwa  kikao hicho cha kazi kitajielekeza kwenye kujadili na kupata majibu ya kutumia mbinu gani kuzuia ukatili wa majumbani kwa watoto na wanawake na pia ni mbinu gani za kunusuru watoto walio wahanga wa ukatili kukimbilia kuishi na kufanya kazi mitaani na wanawaondoaje waliopo mtaani sasa.

“Tujadili na kukubaliana juu ya hatua zipi zinahitajika kuchukuliwa kwenye operesheni ya kudhibiti ukatili majumbani na operesheni ya kuzuia watoto wasikimbilie mitaani na pia operesheni ya kuwaondoa watoto walio mtaani sasa,”amesisitiza

Ameongeza kuwa,  moja ya changamoto za kuendelea kutokea kwa vitendo vya ukatili ni utendaji hafifu wa Kamati za ulinzi wa Wanawake na Watoto hususani kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa pamojana kuwepo kwa Kamati 18,186 nchi nzima.
Kwa upande wake Naibu Waziri, Mwanaidi Khamis amesema kuwa Ukatili unaofanyika ndani ya Jamii, ndio umekuwa unadhorotesha jitihada za Serikali katika Kusukuma gurudumu la Maendeleo kutokana na watu kukatiliwa, hivyo kitendo cha Mhe. Rais kuanzisha Wizara hii, ni hatua kubwa katika kulipa kipaumbele suala lakutokomeza ukatili.

Awali Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk.Zainab Chaula,amesema lengo la kikao hicho ni kutaka kujua mikakati gani waliojiwekewa wadau katika  kukabiliana na vitendo vya ukatili.

“Vitendo vya ukatili vimeongezeka, wadau tupo wapi, watoto wanalala mtaani, Jamii inatakiwa inufaike na uwepo wa Mashirika haya” Dkt. Chaula 
“Kati ya Mashirika elfu 12, ni Mashirika 6000 tu ndiyo yamejitokeza kusema shughuli wanazofanya, hivyo tuliamua kuwa ifikapo tarehe 28 Februari, mwaka huu Mashirika ambayo hayajajitokeza hayatatambuliwa” amesisitiza Dkt. Chaula 
Naye, Kaimu Mkurugenzi Mkaazi wa Plan International Peter Mwakabwale, amesema kuwa  kuna wadau wengi wanatekeleza afua za kukomesha ukatili wa wanawake na watoto lakini hawajakusanya nguvu za pamoja kutekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA)
“Tupo wadau wengi tunaotekeleza afua mbalimbali kutokomeza ukatili kwa Wanawake na Watoto lakini bado kuna changamoto ni muda sasa wa kusimaam pamoja na kuazimia Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto” amesema Mwakabwale
Bw.Mwakabwale amebainisha jitihada zikizofanyika na wadau ni pamoja na kutoa mafunzo kwa wajumbe wa Kamati za MTAKUWWA ngazi zote, kuimarisha huduma za upatikanaji wa Huduma za uzazi na mafunzo kwa Viongozi wa Dini.
Kwa upande wake, Mbunge wa Viti maalum (CCM) Neema Lugangira,amesema kuwa kuna mambo wamebaini kama elimu ndogo ukatili wa kijinsia kwa jamii, madawati ya ukatili yapo ndani ya kituo cha polisi.
“Wakati umefika wa kutambua tatizo la Afya ya akili, Jamii ielimishwe kuhusu kuzungumza na wataalamu wa ushauri nasaha kuhusu changamoto zao”  amesema Mhe.Lugangira 

About the author

mzalendoeditor