Featured Michezo Uncategorized

SIMBA YAIFUATA YANGA ROBO FAINALI KIBABE

Written by mzalendoeditor

…………………………………………….

Na.Alex Sonna

Mabingwa watetezi wa Kombe la Shirikisho la Azam Sports Federation Cup (ASFC) Simba SC wameifuata Yanga Robo Fainali ya Michuano hiyo kibabe kwa kugawa dozi nzito ya mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Simba walianza mchezo kwa kasi huku wakitumia dakika mbili tu kuiadhibu Ruvu Shooting baada ya Yusuf Mhilu kumchongea pasi Bocco akiwa ndani ya 18 na kuunganisha mpira kwa kichwa.

Simba waliendeleza mashambulizi langoni mwa Ruvu Shooting na dakika ya 25 Clatous Chama alifunga  bao la pili akipokea pasi nzuri kutoka kwa Mzamiru Yassin.

Dakika ya 28  Chama tena  akaingia kambani akifunga bao la tatu akipokea pasi kutoka kwa winga Peter Banda na katika dakika ya 40 John Bocco aliwanyanyua tena  mashabiki wake waliojitokeza kushuhudia mchezo huo akifunga bao la nne.

Mashambulizi makali langoni kwa Ruvu Shootingi yalimchanganya beki Michael Masinda baada ya kuunganisha nyavuni krosi ya Gadiel dakika ya 45.

Simba waliendeleza mashambulizi makali langoni kwa Ruvu Shootingi  na dakika ya 45 beki Michael Masinda alijifunga bao la tano akimalizia krosi ya Gadiel dakika ya 45.

Kipindi cha pili kilianza kwa timu zote kufanya mabadiliko huku Simba wakiendelea kuliandama lango la Ruvu Shooting mnamo dakika ya 70 Jimmyson Mwinuke alifunga bao la sita akipokea pasi ya Clatous Chama.

Dakika ya 72 Clatous Chama alipigilia msumari wa saba huku likiwa bao lake la tatu yaani hat-trick akimalizia pasi nzuri kutoka kwa beki Israel Mwenda.

Kwa Matokeo hayo Simba inakamilisha idadi ya timu nane zilizotinga hatua ya Robo Fainali ambazo ni Pamba ambayo ndio timu pekee inayoshiriki Ligi daraja la kwanza iliyofuzu hatua hiyo nyingine saba zote zinacheza Ligi Kuu ya NBC ambazo ni Yanga,Kagera Sugar,Coastal Union,Geita Gold,Azam FC  na Tanzania Polisi.

About the author

mzalendoeditor